PlaneteAfrique
Déconnexion
WS-Apps, le système de gestion de contenus adaptatif développé depuis 15 ans, conçu pour sa puissance, son efficacité et sa simplicité. Trois applications, une présence web maîtrisée :
WS-MySite! Votre présence web immédiate et professionnelle. Découvrir ce pack
WS-Webzine Pour agences de presse et éditeurs. Découvrir ce pack
WS-Ecommerce Vendez en ligne et encaissez par Mobile Money et carte bancaire. Découvrir ce pack

CRDB yatoa zawadi za krismasi kwa wagonjwa Lindi

CRDB yatoa zawadi za krismasi kwa wagonjwa Lindi


Benki ya CRDB Tawi la mkoa wa Lindi imetoa vyandarua hamsini pamoja na vinywaji mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya mkoa huo ya Sokoine ikiwa ni kuungana nao katika kusherehekea sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya.



Akikabidhi  zawadi hizo ikiwa ni pamoja na vyandarua kwa watoto na akina mama wajawazito, sabuni, maji, soda,juisi na vinginevyo, Afisa wa Benki ya CRDB mkoa wa Lindi Abdallah Mohamed amesema ni kawaida ya benki hiyo kufanya hivyo kwa jamii kutokana na faida wanayoipata.



Kwa upande wake, muuguzi msaidizi wa hospitali hiyo Marieta Ng’oge ametoa shukrani kwa Benki ya CRDB na kuomba taasisi zingine kuiga mfano huo.



Kwa upande wao wagonjwa nao wameshukuru na kusema wamejiona ni watu waliojawa na furaha kwani sio kawaida mtu kuacha kufanya shughuli zake na kwenda kuwaona wao.



Martina Ngulumbi, TBC Lindi.




Last Updated ( Monday, 24 December 2012 13:14 )


 

TANZANIE - accès rapides

Actualités par pays

 

Newsletter


 
 
 
 
 
 

Actualités par pays

Newsletter


 
 
 
 
 
Tanzanie - Actualites