PlaneteAfrique
Déconnexion


DC Nachingwea awataka wazazi kuchangia elimu

DC Nachingwea awataka wazazi kuchangia elimu

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Regina Chonjo  amewataka wazazi wilayani humo kuchangia elimu ya watoto wao kwa kuwalipia ada, kununua sare za shule na kufuatilia kwa karibu maendeleo ya masomo yao.



Chonjo  amesema hayo kwenye mahafali ya pili ya shule ya awali ya Kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Nachingwea na kuongeza kuwa ukimsomesha mtoto wa kike ni kufungua ukurasa mpya wa maendeleo katika nchi.



Kwa upande wake Paroko wa Kanisa hilo, Fabian Ng’ombo amesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa miundombinu.



Martina Ngulumbi, TBC Lindi.




Last Updated ( Thursday, 13 December 2012 11:36 )


 
 

Actualités par pays

 
 
 
 

Actualités par pays

Newsletter


 
 
 
 
 
MySite
WS-MYSITE
✨ Présence web
Créez votre site clé en main
Démarrer →
Tanzanie - Actualites